IRINGA: BAADA ya kuteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Klabu za Afrika, Rais wa Yanga, Hersi Said sasa ameteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) na Fainali za Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN).
Uteuzi huo umetangazwa leo Desemba 16, 2023 na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia katika mkutano mkuu wa mwaka wa shirikisho hilo unaofanyika Iringa.
“Kwa nafasi ya kuwa Rais wa klabu Afrika, Hersi Said ni mjumbe wa kamati ya utendaji ya CAF na hivyo ameingia kwenye kamati ya maandalizi ya CHAN na AFCON,” alisema Karia.
Novemba 30, 2023 Hersi aliteuliwa na CAF kuwa Mwenyekiti wa kwanza wa Chama cha Klabu za Soka Afrika katika mkutano uliofanyika ukumbi wa Marriot Mena House, Cairo Misri.