HESLB yazungumzia Samia Scholarship

Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Dk. Bill Kiwia

DODOMA: BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), imewataka wanafunzi na wazazi kupuuzia taarifa inayosambaa katika mitandao ya kijamii na makundi ya ‘WhatsApp’ kuhusu sifa, maeneo ya ufadhili na tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ya Samia Scholarship kwa mwaka 2024/2025.

Taarifa iliyochapishwa katika mitandao rasmi ya kijamii ya HESLB leo Septemba 26, imeitaka jamii kupuuzia taarifa hizo kwa kueleza kuwa siyo taarifa sahihi na inapaswa kupuuzwa.

Advertisement

“HESLB inaendelea kuwasisitiza wanafunzi walengwa na watanzania kwa ujumla kuwa mwongozo na taarifa sahihi kuhusu ‘SAMIA SCHOLARSHIP’ kwa mwaka 2024/2025 zinapatikana kupitia tovuti yake www.heslb.go.tz na kurasa za mitandao ya kijamii kwa jina la HESLB Tanzania,” imeeleza taarifa hiyo ya Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano ya HESLB.

Taarifa hiyo imefafanua kuwa dirisha la maombi ya ‘SAMIA SCHOLARSHIP’ kwa mwaka 2024/2025 lilifunguliwa Agosti 8, 2024 na kufungwa Septemba 14, 2024.

SOMA: HESLB yatangaza fursa