“High-Low” Mitindo ya kisasa na kuvutia

Karibu katika page yetu ya mitindo na Leo tutazungumzia ngua ya high low ambayo inakuwa mbele fupi nyuma ndefu.

Kwenda na wakati ni jambo linalopendwa kufanya mtu kuonekana nadhifu zaidi na wakisasa katika fani ya mitindo na kuvutia.

Mitindo uambatana na Mvaaji anavyovaa vizuri na kuvutia watu kupelekea kuwa nadhifu na yenye kuvutia kwa wanaokuona.

Advertisement

Ili mwanamke uwe wa kisasa, lazima uende na wakati kwa kuvaa nguo zilizopo kwenye chati kwa sasa.

Kama mfuatiliaji sana wa masuala ya mitindo ya Mavazi basi hautakiwa mgeni wa mitindo ya nguo maarufu kama high low.

Vazi hili ni aina ya vazi, ambalo limekuwa maarufu hasa kwa wasichana mjini.Kutokana na ubora wake unaotokana na ushonaji wa nguo hizo.

High low ni aina ya nguo, ambayo mara nyingi upande mmoja huwa mfupi na mwingine mrefu kuzidi mwingine.

Huu ndio ulimwengu wa mitindo na urembo naweza kukwambia mwanamke Fashion dada na kwenda na wakati.

Mbele mara nyingi huwa mfupi na nyuma huwa mrefu ndio maana ya jina la high low ni aina ya nguo ambayo ipo katika mitindo mingi ikiwemo sketi, magauni na mashati Mapana.

Wanawake haswa wasichana wanapenda kuvaa shati la mtindo huo ambapo mara nyingi hupenda kuvalia na taiti. Unapovaa shati ya aina hiyo na (tight) taiti ama kaptura fupi, ambapo vazi hilo mara nyingi kuvaliwa ufukweni.

Nguo hii uweza kuvaliwa popote, mfano kanisani, kazini hata bungeni ambayo unaweza kuvaa na suruali au sketi yenye ufupi wa wastani itapendeza na kuonekana mrembo zaidi endapo sketi itakuwa ya penseli.

Utakapo vaa gauni hilo katika sherehe unaweza kuvaa na kiatu kirefu, kwakuwa mara nyingi sherehe ufanyika usiku unaweza kuvaa gauni la high low fupi kiasi itapendeza na kivutia.

Wanawake wengi hupenda kuvaa gauni la mtindoo huu ili kuonyesha miguuni yao na viatu walivyovivaa, gauni la high low huonyesha mwonekano mzima wa mtu alivyoaa na kupendeza.

Gauni la high low kama ni pana unaweza kuvalia na mkanda mwembamba ili kuweka nakshi ukiongeza na heleni, saa na bangili na cheni pamoja na mtindoo mzuri wa Nywele utakaoweka zitakufanya kutoka Bomba zaidi. SOMA : Rais Samia ampongeza mbunifu wa mavazi Anjali

Kuna sketi aina ya high low ambapo huweza kuvaliwa na blauzi, ambazo unakuja vizuri kwenye mwili na lisiwe shati kubwa sana halitapendeza mara nyingi halipendezi.

Unaweza kuvaa gauni la high low la kukata mikononi na ukavaa na kikoti ukaenda ofisini kiofisi zaidi itapendeza na kuwa nadhifu machoni pa watu.

Kama unapenda high low kwa ofisini nakushairi uvae siku ya ijumaa na sio Jumatatu ukivaa na kiatu kirefu cha wastani pamoja na pochi nzuri itapendeza sana.

High low gauni, sketi na shati kuvaliwa popote inategemea wewe unavaaje na imeshinwaje.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *