DAR ES SALAAM: Leo Septemba 30, 2023 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano (JNICC) katika Jiji la Dar es Salaam, Tanzania inaenda kushuhudia tukio la kisasa na kihistoria kwa Balozi Dk. Salim Ahmed Salim, kuandaa kumbukizi ya maisha yake na mchango wake katika jamii ya ndani na ile ya Kimataifa kupitia mfumo wa Kidigitali (tovuti).
Dk. Salim Ahmed Salim anatambulika kama Mwanadiplomasia wa Kimataifa aliyewahi kushika nyadhifa mbalimbali za kitaifa na kimataifa, ikiwema Waziri wa Mambo ya Nje kuanzia mwaka 1980-1984, Waziri Mkuu wa Tanzania kuanzia Aprili 24, 1084- Novemba 05, 1985, Katibu Mkuu wa Umoja wa Nchi za Afika (OAU) ambayo ni (AU) ya sasa (1989-2001).
Ameandaa historia ya maisha yake na harakati zake katika siasa, diplomasia na utumishi wa umma na harakati za ukombozi za Uhuru wa Bara la Afrika, aliouandaa kupitia tovuti maalumu yenye masimulizi yanayoshereheshwa na matumizi ya picha mnato na picha mjongeo.
Dk. Salim, ni mwanasiasa kutoka Tanzania, amezaliwa Januari 23, 1942 huko Zanzibar kipindi cha Utawala la Sultan. Ameishi katika duru za kidiplomasia tangu miaka ya 1960.