HOSPITALI ya Rufaa ya Mkoa wa Arusha (Mount Meru) inatarajia kusimika vifaa vya hewa tiba ya oksijeni ifikapo Machi mwaka huu ili kusaidia kuokoa maisha ya wagonjwa hususan kwa watoto ,watu wazima na wengineo .
Hayo yamesemwa jijini Arusha na Maganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Arusha,Dk Alex Ernest wakati akitoa taarifa ya miezi mitatu ya hali ya utendaji kazi na utoaji huduma katika hospitali hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Amesema lengo la serikali kusimika mitambo hiyo ya kisasa ni kuwezesha kuokoa gharama kubwa ya huduma hiyo pindi itakapohitajika kwa udharura wake
Amesema uwepo wa mitambo hiyo ya oksijeni itawezesha hospitalu hiyo na serikali kutumia gharama ya sh, milioni 60 hadi 90 kwa kipindi cha miezi mitatu kwaajili ya kununua hewa hiyo ili kusaidia wagonjwa wanaohitaji kuwekewa.
“Usimikwaji wa vifaa vya hewa tiba utaokoa gharama kubwa tunazotumia kwaajili ya kutoa huduma kwa wananchi lakini pia tunaanza ujenzi wa kliniki ya ugonjwa wa kansa ili kuondoa changamoto ya wagonjwa kupata huduma hiyo nje ya mkoa wa Arusha”