Hotuba Makamba miaka 74 ya kuanzishwa kwa PRC
Oktoba 1, 2023 ni maadhimisho ya hatua muhimu katika historia ya China na watu wake, na pia katika uhusiano kati ya mataifa yetu mawili makubwa.
Nawaletea salamu za dhati kutoka kwa MHE. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Serikali na wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (URT), kwa Serikali na Jamhuri ya Watu wa China (PRC). Tunatoa pongezi zetu za dhati na kuwatakia kila la heri katika hafla hii ya kihistoria.
Kando na kuungana nawe na watu wa China kote duniani kusherehekea siku hii ya kihistoria, hafla ya kuadhimisha miaka 74 tangu kuanzishwa kwa PRC inatupa fursa nyingine ya kutafakari juu ya ushirikiano wetu, na kuthibitisha dhamira yetu ya kuimarisha zaidi uhusiano wa karibu na wa kihistoria wa urafiki na ushirikiano uliopo kati ya nchi zetu mbili na watu wetu.
Ni katika ari hii, MHE. Rais Samia Suluhu Hassan anathamini uhusiano mzuri na wa kirafiki uliopo kati ya nchi zetu mbili, na anapongeza dhamira ya MHE. Xi Jinping, Rais wa PRC katika kuimarisha uhusiano na ushirikiano kati ya nchi zetu mbili.
MHE. Rais Samia Suluhu Hassan, anapenda kumhakikishia MHE. Rais Xi Jinping kwa di dhamira yake binafsi ya kuimarisha mahusiano haya zaidi. Safari ya China tangu kuanzishwa kwake imekuwa ya mafanikio sana.
Katika kipindi cha miaka 74 iliyopita, PRC imefanya mabadiliko ya makubwa, kutoka taifa maskini na dhaifu kiuchumi, hadi mojawapo ya uchumi unaoongoza duniani na taifa lenye nguvu duniani.
Kwa miaka mingi, ukuaji wa kasi wa uchumi wa China umetoa mchango mkubwa katika maendeleo ya dunia, uimarikaji wa uchumi na ukuzaji uchumi.
Mchango wa China katika kuondoa umaskini duniani hauwezi kupuuzwa. Katika nyanja za kimataifa, tunaipongeza China kwa kushiriki na kuheshimu taratibu za ushirikiano katika Nyanja za kimataifa, na ushiriki katika mambo ya kimataifa, jambo ambalo limekuwa nyenzo muhimu katika utatuzi wa changamoto za kimataifa, kama mbadiliko ya tabia nchi, kupambana na umasikini na kulinda Amani.
Safari ya mafanikio ya China ni uthibitisho wa uthabiti, azma, maono, uongozi, na bidii na dhamira thabiti ya watu wa China kutaka maendeleo na kusonga mbele, na ni chanzo cha hamasa kubwa sote kwetu sote. Hii ni alama kubwa ya mafanikio yanaweza kupatikana kwa nchi kama zitashikamana pamoja ili kutimiza lengo moja.
Napenda kuchukua fursa hii kuipongeza Serikali na Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) kwa maendeleo makubwa yaliyopatikana katika miaka hii 74.
CPC na Serikali zimeongoza njia ya China kuelekea maendeleo ya kisasa, kufikia ukuaji wa haraka wa uchumi pamoja na utulivu wa muda mrefu wa kijamii. URT na PRC zina historia ndefu ya urafiki na ushirikiano.
Siku zote tumekuwa tukifupisha uhusiano wetu katika sentensi moja “Tanzania na China ni ‘marafiki wa nyakati zote’”, kuonyesha jinsi mataifa yetu yalivyoshirikiana bega kwa bega kwa miaka mingi. Urafiki na ushirikiano wetu umejengwa katika msingi imara na urafiki kati ya waasisi wa mataifa yetu mawili: Hayati Mwenyekiti Mao Tse Tung na Waziri Mkuu Zhou Enlai kwa upande wa China na Hayati Rais Julius Kambarage Nyerere na Hayati Abeid Amani Karume kwa upande wa Tanzania.
Ni kutokana na msingi huo imara, vizazi na vizazi vya mataifa yetu mawili vimeweka uzito mkubwa juu ya umoja na mshikamano. Kwa hiyo, mahusiano haya ya kindugu yamekuzwa, kuunganishwa na kuendelezwa na vizazi vilivyofuatana vya viongozi katika mataifa yetu mawili baada yao.
Tunasherehekea kumbukumbu ya miaka 74 ya kuanzishwa kwa PRC ikiwa ni chini ya mwaka mmoja tangu MHE. Rais Samia Suluhu Hassan alipofanya ziara ya kihistoria nchini China Novemba 2022, kwa mwaliko wa MHE. Rais Xi Jiping.
Rais Samia ni Mkuu wa Nchi wa kwanza wa Afrika kuzuru China baada ya Mkutano Mkuu wa 20 wa Kitaifa wa CPC. Ziara hii ya kihistoria imeimarisha ushirikiano wetu na kuongeza uelewa wetu wa vipaumbele na changamoto za kila mmoja wetu.
Ilitoa mwanya kwa Rais Xi Jinping na Rais Samia Suluhu Hassan kusisitiza dhamira yao thabiti ya kuimarisha uhusiano wetu wa pande mbili kwenye Ushirikiano Mpana wa Kimkakati wa Ushirika na kukubaliana kuendeleza ushirikiano wa Tanzania na China katika maeneo yote.
Tunaposherehekea kuanzishwa kwa PRC, tunatafakari pia juu ya uhusiano wa kina kati ya nchi zetu mbili. Uhusiano wetu baina ya nchi hizi mbili umeendelea kuwa na guvu zaidi na zaidi kwa miaka mingi, ukihusisha maeneo mbalimbali kama vile kilimo, afya, elimu, ulinzi, biashara, uwekezaji, utamaduni na mabadilishano ya watu na watu, miundombinu hasa Reli ya Tazara, ambayo ni alama ya mshikamano kati ya mataifa ya Afrika na China.
Mwaka huu, tunaadhimisha miaka 10 ya mpango wa ushirikiano wa kikanda (BRI) wa China ambao ulianzishwa mwaka 2013.
Mpango huo ulioanzishwa ili kusaidia uunganishaji wa miundombinu na kuchochea ukuaji wa biashara na uwekezaji, umetoa fursa mpya za ushirikiano kati ya mataifa yetu mawili.
Tanzania inaunga mkono kikamilifu mradi huu adhimu, na kusisitiza dhamira yake ya kuendelea kuunga mkono Mpango huo na kushiriki katika shughuli zake husika ikiwa ni pamoja na Mkutano wa Tatu wa Ukanda na Njia kwa Ushirikiano wa Kimataifa utakaofanyika mwezi ujao mjini Beijing.
Tunaamini kwamba kupitia uunganishaji wa miundombinu imara na kuongezeka kwa biashara, tunaweza kufungua uwezo kamili wa uchumi wetu na kuboresha maisha ya watu wetu.
Pia tunatarajia kuimarisha ushirikiano wetu wa kiuchumi ambao umekuwa msingi wa uhusiano baina ya Tanzania na China. Kwa miaka mingi, ushirikiano huu umeifanya China kuibuka kuwa miongoni mwa washirika wakubwa wa kibiashara wa Tanzania na wawekezaji wa nje, hivyo kuchangia pakubwa katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya nchi zetu.
Tunapoadhimisha miaka 74 tangu kuanzishwa kwa PRC, ni vyema kutambua pia kwamba mwaka huu pia ni mwaka muhimu katika historia ya Tanzania na China, ikiwa ni mwaka wa 10 tangu MHE. Rais Xi Jinping alipofanya ziara yake ya kwanza barani Afrika, na Tanzania ikiwa ni kituo chake cha kwanza.
Ni kupitia ziara hiyo MHE. Rais Xi Jinping alitoa kanuni ya uaminifu, matokeo halisi, upendo na imani nzuri ya kuongoza ushirikiano kati ya China na Afrika. Muongo mmoja baadaye, sifa hizi muhimu za uhusiano kati ya China na Afrika zimeongoza kwa mafanikio ushirikiano kati ya China na Tanzania na ninaamini utaendelea kwa miongo kadhaa ijayo.
Bila kusahau, mwakani Tanzania na China zitaadhimisha hatua nyingine muhimu ya kihistoria, miaka 60 ya Uhusiano wa Kidiplomasia. Kwa hakika tunatazamia sherehe hii kubwa ili kuadhimisha mahusiano yetu ya kindugu ya muda mrefu.
Tunapotazamia siku zijazo, tuna uhakika kwamba uhusiano wetu baina ya nchi mbili utaendelea kustawi na kuimarika.
Tutaendelea kuwa na ushirikiano wa kimkakati, kuimarisha na kupanua mahusiano na ushirikiano wetu mbali na kwa pande zote; kuongeza urafiki na uaminifu kati ya watu wetu wawili; kufanya kazi pamoja kukuza amani ya kikanda na kimataifa, utulivu na ustawi; na tutaendelea kujifunza kutokana na uzoefu na utaalamu wa kila mmoja wetu ili kuhakikisha ushirikiano wetu wa nchi mbili katika nyanja zote na ngazi zote unakuwa na mafanikio makubwa.
Nataka kuongeza kidogo, kama mnavyojua uzoefu wangu binafsi kuhusu uhusiano kati ya watu na watu kati ya nchi zetu mbili. Baadhi yenu mnajua kwamba kwa miaka miwili kati ya 2019 na 2021, nilikuwa nje ya Serikali na nilichukua muda wa kusafiri.
Nilisafiri sana nchini China mnamo Novemba 2019 kwa wiki mbili. Nilichukua ndege, nilichukua treni, nilipita katikati ya nchi na China vijijini, nikijaribu kuelewa ni nini kinachoifanya China iwe katika mwelekeo ambao inakwenda katika hali ya ustawi, na nilikuwa peke yangu, hakukuwa na itifaki na nilichagua kufanya hivyo ili kujifunza ushiriki wa watu kwa watu. Nilikaa vijijini.
Niseme kwamba nilikaribishwa sana na Wachina katika maeneo niliyokwenda, na hata kule China vijijini unaposema unatoka Tanzania, mara moja wanaitambua Tanzania na mambo mawili yanawajia akilini: moja ni Julius Nyerere, nyingine ni Tazara, kama alama ya ushirikiano.
Kwa hiyo nilipata kufahamu jinsi watu wa China kote nchini wanavyofahamu ushirikiano wa muda mrefu kati ya nchi zetu mbili na watu ambao umedumu kwa muda mrefu.
Nilipoingia katika viwanja hivi, nilipata fursa ya kuangalia maonyesho kuhusu misheni ya matibabu kwa miaka mingi ambayo imekuwa ikija nchini kwetu kutoka China na unaweza kuona dhamira ya serikali ya China na watu kufanya kazi nasi , kuwa nasi, katika safari yetu ya ustawi na maendeleo.
Kwa hivyo, hili linathaminiwa, na sisi pia kama nilivyotaja tukiongozwa na mwelekeo ya China katika maendeleo ya vijijini na maendeleo ya mtaji wa watu.
Tunazungumza kuhusu malengo ya maendeleo endelevu, na mafanikio ya malengo ya maendeleo ya milenia (MDGs) katika kuwaondoa watu kutoka kwenye umaskini hadi kwenye ustawi, lakini sote tunajua kwamba mafanikio makubwa zaidi ya watu kutoka umaskini kwenda kwenye ustawi ilitokea nchini China.
Mchango wa China katika mafanikio ya MDGs hauwezi kupuuzwa. Na huu ndio ukweli ambao sote lazima tukumbuke kila wakati. Kwa hiyo, tunasherehekea kama Watanzania, urafiki ambao tunashirikiana na Wachina wanaoishi kati ya watu wetu na wanaofanya biashara hapa Tanzania. Tanzania ni