Ibrahimovic amlipua Ten Hag

MKONGWE Zlatan Ibrahimovic ameonesha kutokukubaliana na uwepo wa kocha Eric Ten Hag katika klabu ya Man United, akieleza kuwa kocha huyo hana uzoefu wa kufundisha klabu kubwa.
“Je, uzoefu wa kocha huyu ni upi? kijana mwenye kipaji kisha anakuja United… Man United wana mawazo tofauti, wachezaji tofauti”. “Unakuja United, unafanya hivyo hivyo”, Zlatan alisema kwenye mahojiano na mwandishi wa habari, Piers Morgan.
Nyota huyo wa zamani wa United alisema: “Kutoka Ajax kuja United kama alivyofanya ni tofauti kubwa – nimekuwa katika klabu zote mbili. “Una aina tofauti ya nidhamu.
“Ajax ni klabu yenye vipaji. Wana vipaji bora katika klabu. Hawana nyota wakubwa.
Katika suala la kumpa muda Ten Hag, Ibra alisema: “Unampa kocha muda gani, inategemea na wamiliki wanataka nini, lakini ukiwasikiliza mashabiki, muda mwingi wanataka kushinda, nawaelewa kwa sababu wamezoea kushinda.”



