Sina mpango wa kuacha muziki

MSANII wa muziki anayefahamika kwa jina la Haroun Rashid maarufu kama Inspekta Haroun Babu ameweka wazi matarajio yake ya kuendelea kufanya kazi na wasanii mbalimbali wanaofanya vizuri katika muziki wa Bongo Fleva kwa sasa.
Akizungumza na HabariLEO, Inspector Haroun Babu alisema tayari ana miradi kadhaa ya muziki inayoendelea, huku mingine ikiwa imekamilika. Amesema miongoni mwa wasanii anaotarajia kufanya nao kazi ni Country Boy, G Nako na Jux.
Aidha, msanii huyo alizungumzia tetesi zinazodai kuhusishwa kwake na kampeni mbalimbali, ikiwemo zinazohusu masuala ya muziki na siasa. Ameweka wazi kwamba hahusiki na kampeni yoyote na hana uhusiano wowote na chama chochote cha siasa. βSijihusishi na siasa kwa namna yoyote ile, sina chama wala kampeni yoyote,β alisema Inspector Haroun Babu.
Katika hatua nyingine, amekanusha madai kuwa anajiandaa kuacha muziki, akibainisha kuwa bado ana hamu kubwa na anaiona tasnia ikimhitaji. βSina mipango ya kuacha muziki kwa sababu bado naona muziki unaniitaji,β alisema. SOMA: Stara: Sitaacha kuimba nyimbo za zamani




β 彑[ππππ ππππππ π ππ ππππ ππππ ππππππ ππππ]彑β
Start making cash right nowβ¦ I get paid over $220 per hour working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my befst friend earns over $19,000 a month doing this and she convinced me to try. ift was all true and has totally changed my lifeβ¦ This is what I do, check it out by visiting Following Linkβ¦
πππ«π π’π¬ π π¬πππ«πππ=========> https://bs786s.blogspot.com/