iRAN imegoma kurejea kwenye mazungumzo

TEHRAN : WAZIRI wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, amesema hakuna uwezekano wa nchi yake kurejea katika mazungumzo na Marekani kwa sasa, hadi pale itakapohakikishiwa usalama na kutoshambuliwa tena.

Akizungumza na kituo cha CBS Evening News cha Marekani, Araghchi alieleza kuwa pamoja na matamshi ya Rais wa Marekani, Donald Trump, kwamba mazungumzo ya nyuklia yanaweza kuanza tena mapema wiki hii, Iran bado inahitaji muda zaidi kabla ya kujihusisha tena katika mazungumzo hayo.

“Hatufungi milango ya diplomasia, lakini hatutarudi mezani bila uhakikisho wa kiusalama,” alisema Araghchi katika mahojiano hayo maalum. SOMA: Mpango wa Nyuklia Iran watingisha Marekani

Kauli hiyo inakuja baada ya hali ya mzozo kati ya Iran, Israel na Marekani kuzidi kuwa tete, kufuatia mashambulizi yaliyofanywa na Israel dhidi ya maeneo ya nyuklia ya Iran, huku Marekani ikishiriki kwa kulipua maeneo ya Fordo, Natanz na Isfahan mnamo Juni 21.

Mazungumzo kati ya Iran na Marekani kuhusu mpango wa nyuklia yalivunjika kufuatia mashambulizi hayo, na sasa matarajio ya kurejea mezani yanaonekana kusuasua.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button