Jafo ashiriki ugawaji tuzo wafanyabiashara Kariakoo

DAR ES SALAAM: WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Dk Selemani Jafo, ameshiriki zoezi la ugawaji wa tuzo kwa wafanyabiashara wa soko la Kariakoo ambapo alitoa pongezi kwa uongozi na waandaaji wa tuzo hizo kwa ubunifu.
Amesema hatua hiyo ni chachu ya kuwahamasisha wafanyabiashara kuwa makini na kuongeza ubora wa huduma zao.
Akizungumza baada ya kupokea tuzo, mmoja wa washindi, Eunice Bushanga, ambaye ni Mkurugenzi wa Mwangaza Stationery & Supply, alisema kuwa mchakato wa utoaji wa tuzo hizo ulikuwa wa haki na ulijumuisha watu wengi, hivyo hapakuwa na upendeleo wowote.
Tuzo hizo zinalenga kutambua mchango wa wafanyabiashara katika kukuza uchumi wa nchi na kutoa motisha kwa wengine kufanya kazi kwa bidii na ubunifu