Jafo awaagiza wakuu wa mikoa kutenga maeneo ya uwezekaji viwanda

Waziri wa Viwanda na Biashara .Dkt.Selemani Jafo alipotembelea sehemu za Kiwanda cha Balochistan Group of Industry Limited (BGI) Mkuranga Mkoani Pwani(Picha:Wizara Viwanda na Biashara)

MKURANGA: WAZIRI wa Viwanda na Biashara Dkt Suleiman Jafo amewaagiza wakuu wote wa mikoa nchini kuhakikisha wanatenga maeneo ya uwekezaji wa viwanda wakati serikali ikiendelea kuhamasisha wawekezaji wengi zaidi kuja nchini.

Waziri Jafo amesema hayo leo alipotembelea Kiwanda cha Balochistan Group of Industry Limited (BGI) kilichopo Mkuranga mkoani Pwani.

“Ni muhimu wenye viwanda kufahamu kuwa, ajira ni jambo la msingi na kuhakikisha wanaangalia maslahi ya wale wanaowasaidia kufanya kazi katika maeneo yao,” amesema Jafo.

Advertisement

Soma hapa: http://Wizara ya Viwanda yaomba kuidhinishwa Sh bil 110.9

Waziri Jafo alipatiwa maelezo kuhusu ufanyaji kazi wa Kiwanda hicho kinachohusika na utengenezaji wa waya za shaba, sufuria na urejeshaji wa betri za magari na Mtendaji Mkuu wa Kiwanda hicho, Khudadad Bizanto

Kwa upande wake, Mkuu wa wilaya ya Mkuranga, Hadija Nasri ameiomba serikali kutoa uangalizi wa pekee kwa wilaya hiyo hasa kwenye miundombinu ili kuvutia zaidi wawekezaji.