Jaji Chande ataja sababu tume kuongezewa muda

DAR ES SALAAM: Mwenyekiti wa Tume ya Uchunguzi wa Matukio ya Uvunjifu wa Amani ya wakati na baada ya uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 Jaji Mstaafu Othman Chande ametaja sababu nne za tume hiyo kuongezewa muda wa siku 21.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Chande alisema sababu ya kwanza ni ushahidi kuendelea kuongezeka, pili ni ushauri wa kitaalamu ambao wameuomba, pia kuchambua kwa kina ushahidi mwingi walioupata.

Ametaja sababu nyingine kuwa ni kuhakikisha ripoti ikitoka inakuwa kwenye mfumo wa lugha ya Kingereza.

Aidha, alikanusha uvumi unaonezwa katika mitandao ya kijamii kuwa tume hiyo imeongezewa muda wa siku 21 ili kurekebisha taarifa yake kwa kuchakachua baadhi ya taarifa.

“Tume imeongezewa muda kwa sababu nne; Moja ni ushahidi mwingi unaoendelea kuingia hivi sasa na pili ni ushauri wa kitaalamu ambao tumeomba na wataalamu wa sayansi wanaendelea kutupa, tatu ni kuchambua kwa kina ushahidi mwingi ambao tumeupata na mwisho ni kuhakikisha kwamba ripoti ikitoka inatoka kwa lugha mbili za mpigo yaani Kiingereza na Kiswahili ili kila mwananchi aelewe.”

Amekaririwa Jaji Mstaafu Othman Chande. Chande amebainisha kuwa sababu hizo zipo hadharani na zimetangazwa kwenye gazeti la serikali na amewahakikishia watanzania kuwa hawapaswi kuwa na hofu kuhusu uadilifu wa ripoti hiyo, akisisitiza kuwa tume hiyo inafanya kazi kwa uhuru bila shinikizo la nje. zilizosababisha vifo vya watu kadhaa na uharibu mkubwa wa mali zikiwemo ofisi za umma, vituo vya mafuta na vituo vya polisi.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button