Jaji Chande: Ripoti itawafariji waathirika Oktoba 29

DAR ES SALAAM: MWENYEKITI wa Tume ya Kuchunguza Matukio ya Oktoba 29, Jaji Mkuu mstaafu, Mohamed Chande Jaji Chande amesema tume inaamini ripoti itakayotoka itawafanya waathirika wa ghasia za Oktoba 29, kujihisi wametendewa haki kwa kiasi kikubwa.

“Tunataka ripoti ikitoka waathirika wa matukio ya Oktoba 29 wajione wamo ndani ya ripoti. Tunataka baada ya matokeo ya Tume twende mbele kama taifa,” alifafanua Jaji Chande.

Alifafanua Watanzania na jumuiya ya kimataifa wana matumaini makubwa na matokeo ya tume, hivyo wana deni kuhakikisha wanafanya kazi hiyo kwa weledi bila kuacha ushahidi.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button