Jasinta Makwabe: Someni kabla ya kuingia mitindo

Mwanamitindo Jasinta Makwabe

MWANAMITINDO Jasinta David Makwambe amewashauri vijana wanaotamani kuingia kwenye sekta ya Mitindo kusoma kwanza ili kutumia elimu watakayopata kufanikisha ndoto zao.

Makwabe amesema anaamini zaidi kwenye elimu na kwamba vijana kuingia kwenye mitindo wakiwa na elimu itawasaidia kufanya vizuri zaidi.

Advertisement

“Mimi nimefanya vitu vyote hivyo nikiwa shule, nimeanza nikiwa shule, wasiache shule kwa sababu ya kuingia kwenye mitindo, wanaweza kufanya wakiwa wanasoma wakiwa na nafasi ila hiyo ni chuo maana ndio unaweza kufanya ukiwa huru,” amesema Makwabe.

SOMA: Wanamitindo watakiwa kuongeza ubunifu

Akizungumzia wanamitindo waliomvutia kuingia kwenye sekta hiyo, Makwabe amewataja Flaviana Matata, Miriam Odemba kuwa ni miongoni mwa wanamitindo waliofanikisha uwepo wake kwenye eneo hilo.

Ametaja wanamitindo wa nje kuwa ni Naomi Campbell, mwanamuziki Rihanna na wengine. Amesema tofauti na uanamitindo yeye ni mfanyabiashara.

Novemba 25 mwaka uliopita Jasinta Makwabe aliiwakilisha Tanzania kwenye mashindano makubwa ya Future Face 2023 yaliyofanyika Nigeria.

/* */