Jinsi ya kutunza nywele za asili

Nywele za asili ambazo hazijawekwa dawa zinakuwa ndefu au fupi. Nywele zisizo na dawa zikituzwa huwa zinapendeza na kuvutia zaidi.zikiwa na mitindo yoyote Kutunza Nywele za asili na zile zenye dawa mara nyingi huwa ni tofauti sana.

Zingatia kutunza na kutengeneza Nywele ziwe za tofauti na ulivyozoea kuweka ili iweze kuweka staili tofauti na kwenye ubora unaotakiwa.Kwanza kabisa unatakiwa kutunza Nywele zako kwa kuosha na kuziweka sawa kwa kutumia shampoo iliyotengenezwa kwaajili ya Nywele zisizo na dawa kama utatumiwa ya Nywele zenye dawa basi itaweka condition.

Hii inasaidia Nywele kuwa laini na kuzuia zisiwe kavu baada ya kuosha.

Advertisement

Pili unatakiwa kupaka mafuta ya maji ili kuleta unyevunyevu na Nywele kungara.

Unaweza kutumia mafuta ya Nazi, jojoba, mnyonyo au mzaituni.Mafuta haya husaidia kulainisha ngozi ya kichwa kufanya Nywele kuwa vizuri na kuzuia mbu kichwani na kuepuka Nywele kuwasha washa.

Usitumie mafuta ya mgando maana hutengeneza mba kichwani kwenye Nywele za asili ambayo kupelekea miwasho.

Usisahau kufanya steming kwa mwezi mara moja au mbili zinasaidia kukuza Nywele, unaweza kuweka steming kwa kutumia mayai husaidia zaidi kurutumisha Nywele.

Pia unaweza kutumia tui la Nazi, kiini cha yai, unaweza kuchanganya ukaweka kwa pamoja koroga kisha unatakiwa kupaka  kwenye ngozi ukimaliza vaa kofia ya plastiki Kaa nayo dk 45 na baadae osha Nywele zako husaidia Nywele kuwa nzito na yenye ubora zaidi.

Wakati wa usiku ukienda kulala unatakiwa kuzisuka Nywele zako mabutu ili zisijifunge wala kujisokota kisha vaa kofia inasaidia Nywele zisikatike. SOMA : Kuna shida watoto Kusuka?

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *