JK aongoza mahafali ya 17 MUCE

IRINGA;Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Rais mstaafu wa Awamu ya Nne  Dk Jakaya  Kikwete, ameongoza mahafali ya 17 ya Chuo Kishiriki cha Elimu Mkwawa (MUCE) mjini Iringa leo, ambapo ametunuku shahada mbalimbali za umahiri na za awali kwa wahitimu.

Katika ngazi ya umahiri, amewatunuku Digrii ya Umahiri wa Sayansi na Ualimu (Master of Science with Education) kwa wahitimu wanne, Joyce Dismas, Osia  Mwanyesya, Deogras mmanuel na Samwel  Lungo.

Aidha, wanafunzi wawili, Mbazi  Senkondo na Joseph Luoga—wamepata Digrii ya Umahiri wa Sayansi katika Ubunifu wa Kihisabati (Master of Science in Mathematical Modelling), huku John Ngazime Josephat akitunukiwa Digrii ya Umahiri wa Elimu Jamii na Ualimu (Master of Arts with Education).

Kwa upande wa Shahada za Awali, jumla ya wahitimu 565 wamepata Digrii ya Awali ya Elimu Jamii na Ualimu (Bachelor of Arts with Education). Wahitimu wengine 365 wametunukiwa Digrii ya Elimu katika Sayansi (Bachelor of Education in Science), 334 wakipewa Digrii ya Awali ya Sayansi na Ualimu (Bachelor of Science with Education), na 17 wakitunukiwa Digrii ya Awali ya Sayansi katika Kemia (Bachelor of Science in Chemistry).

Katika kilele cha hafla hiyo, Mkuu wa Chuo amekabidhi pia Cheti cha Ubora kwa mhitimu aliyeng’ara zaidi, Lekishin Koipa, aliyepata ufaulu wa daraja la kwanza kwa wastani wa GPA 4.8—ikiwa ndiyo alama ya juu zaidi miongoni mwa wahitimu wote wa MUCE mwaka 2025.

Habari Zifananazo

3 Comments

  1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
    .
    This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com

  3. Google provides awesome remote work opportunities, allowing me to earn $2000-$3000 weekly with just 2-4 hours of daily work. It’s been a game-changer, offering flexibility and reliable income. If you’re seeking a genuine way to earn online, don’t miss this chance. Start today and transform your life!
    .
    More Details For Us →→ http://www.big.income9.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button