JKT Stars, Vijana kuisaka fainali kikapu leo

TIMU za mpira wa kikapu za wanawake, JKT Stars na Vijana Queens zinatarajiwa kucheza mchezo wa pili hatua ya nusu fainali, Ligi ya Kikapu mkoa wa Dar es Salaam leo usiku.

JKT Stars tayari imeshinda mchezo wa kwanza kwa pointi 66-61 katika mchezo uliokuwa na ushindani mkali.

Advertisement

Bado kazi ipo, iwapo JKT itashinda itaingia fainali lakini ikipoteza wote watasubiri mchezo wa mwisho wa kuamua mshindi atakayesonga mbele.

SOMA: Dar City, JKT Stars hazikamatiki

Mshindi wa mchezo huu atamenyana na mshindi wa mechi kati ya Don Bosco Lioness dhidi ya DB Troncatti.

Katika nusu fainali ya kwanza Don Bosco Lioness ilishinda kwa pointi 63-57 kwenye Uwanja wa Don Bosco Oysterbay. Mchezo wa pili Troncatti ikashinda pointi 64-45.  Mchezo wa tatu kesho utaamua mshindi.

Kwa upande wa wanaume, UDSM Outsiders ilishinda mchezo wa kwanza kwa pointi 62-50, kisha Savio ikashinda mchezo wa pili kwa pointi 56-51. Mchezo wa tatu kesho utaamua wa kucheza fainali.