WILAYA ya Kahama iliyopo mkoani Shinyanga imetajwa kuwa kinara wa utoroshwaji madini nje ya nchi hivyo kuikosesha mapato serikali.
Waziri wa Madini, Anthony Mavunde ametoa taarifa hiyo jana katika hafla akifungua kikao kazi cha maofisa madini wakazi sambamba na maofisa kutoka Wizara ya Madini jijini Tanga.
SOMA: Mavunde atoa maelekezo 5 kwa Stamico
Kufuata hali hiyo amewaelekeza maofisa madini wakazi waliopo kwenye mikoa yote nchini kuongeza kasi ya kudhibiti utoroshwaji wa madini nchini.
“Watoroshaji wanambinu nyingi kama kule Kahama wao wanatumia mashine za kuchakata wa mpunga Ili kufanya utoroshwaji huo hivyo tuongeze mbinu za kudhibiti kwa kuzihusisha vikosi kazi vilivyopo kwenye maeneo yenu,” amesema Waziri Mavunde.