‘Kama humuoni ndugu yako toa taarifa’
MANYARA: Hanang. Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang mkoani Manaya, Rose Kamili, amewataka wananchi ambao hawafahamu ndugu zao walipo kutokana na mafuriko yaliyotokea usiku wa kuamkia leo eneo la Katesh wilayani Hanang watoe taarifa haraka.
Kamili amezungumza hayo muda mfupi uliopita katika Kijiji cha Gendabi, wilayani Hanang, wakati wa mkutano wa hadhara na wananchi wa eneo hilo kuhusu athari za mafuriko hayo na kueleza kuwa hiyo itasaidia katika juhudi za uokoaji.
Hata hivyo baada ya tangazo hilo la Mwenyekiti huyo wa halmashauri hakukuwa na mwanakijiji yeyote aliyejitokeza kupotolewa na ndugu, badala yake walisema hofu yao ni upande wa pili wa kijiji hicho ambapo wanatenganishwa na mto.