‘Kama unaweza kumfunga Yanga 4 yeye atakufunga 6’

ARUSHA: Kocha wa Ihefu Fc Mecky Mexime amesema ili kujisifu una timu bora ni lazima ucheze na timu yenye bora kama ambavyo yeye na vijana wake wapo tayari kucheza dhidi ya Yanga kesho kwenye mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la CRDB.

Mexime ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumzia maandalizi ya mcheoz huo ambapo amesema anafahamu ubora walionao Yanga lakini wachezaji wake hawapaswi kuingia kinyonge katika mchezo huo.

“Watu wengi wanawapa sana nafasi Yanga kutokana na washakuwa mabingwa na kweli wana timu bora lakini na sisi tumeitengeneza timu yetu , sasa ukitaka kuifunga timu bora lazima na wewe timu yako iwe bora kwahiyo na sisi tuna timu bora,” amesema Mexime na kuongeza

Isome pia https://www.instagram.com/p/C7G8-ctopc9/?utm_source=ig_web_copy_link&igsh=MzRlODBiNWFlZA==

“Yanga yeye anajiamini ana watu wanaweza kuimaliza mechi ,haangalii utamfunga ngapi huwa anaaangalia atakufunga ngapi kama unaweza kumfunga nne yeye atakufunga sita, kwahiyo inabd tuangalie tutacheza vipi karata zetu, “amesema kocha huyo.

Mchezo huo wa Nusu Fainali ya pili utapigwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha majira ya 9:30 alasiri.

 

Habari Zifananazo

Back to top button