Kasulu yatumia 4R uandikishaji uchaguzi mitaa

HALMASHAURI ya Wilaya ya Kasulu imesema kuwa 4R za Rais Samia ni miongoni mambo manne yaliyoifanya halmashauri hiyo kufanya vizuri kwenye zoezi la uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura.

Imeelezwa kuwa Mkoa wa Kigoma umefikisha asilimia 99.7 ya uandikishaji wa wapiga kura katika daftari la wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Msimamizi wa Uchaguzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, Dk.Semistatus Mashimba amesema hayo alipozungumza na waandishi wa habari wakati akitoa tathmini ya zoezi zoezi la uandikishaji.

Advertisement

SOMA: Uchaguzi mitaa kutoa viongozi bora

Dk. Mashimba amesema miongoni mwa mambo hayo mambo ni ushirikiano uliokuwepo baina ya wasimamizi wa zoezi hilo kutoka Halmashauri ya Wilaya Kasulu wakiongozwa na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Dk.Mashimba, viongozi wa vyama vya siasa, viongozi wa dini, wazee maarufu, vijana na vikundi vya Sanaa.

Msimamizi huyo wa uchaguzi amesema kuwa 4R za Rais Samia zinazoakisi katika  maridhiano, mabadiliko, ustahimilivu na kujenga upya zimewezesha makundi mbalimbali kufanya kazi pamoja ikiwemo vyama  vyote vya siasa.

Sambamba na hilo kufika mapema kwa vifaa kwa ajli ya zoezi la uandikishaji na fedha za uhamasishaji ni miongoni mwa mambo yaliyochangia kufanikiwa kwa zoezi hilo kwenye halmashauri hiyo ikiwa ni Pamoja na kuzingatia miongozo na kanuni zilizoratibiwa na Wizara ya Tamisemi chini ya Wazir, Mohamed Mchengerwa.

SOMA: Kiongozi ACT ajiandikisha uchaguzi mitaa

Oktoba 11 mwaka huu akizungumza wakati wa uzinduzi wa zoezi la uandikishaji wapiga kura katika daftari la wapiga kura la mkazi kwa ajili ya uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa Katibu Tawala wa Kigoma, Hassan Ruga alisema kuwa Kigoma ulitarajia kuandikisha wapiga kura milioni 1.3 kupitia vituo 2252 vilivyotengwa mkoani humo.