Kidato cha tano kuanza Agosti

Tamisemi yaanika shule, vyuo walivyowapangia

WANAFUNZI  1,878 wakiwemo wasichana 1,097 na wavulana 781 wamepangiwa katika shule za sekondari maalum nane ambazo ni Kilakala, Mzumbe, Ilboru, Kisimiri, Msalato, Kibaha, Tabora Boys na Tabora Girls.
Wanafunzi  hao 188,128 waliokidhi vigezo wamechaguliwa na kupangiwa kujiunga na kidato cha tano katika shule mbalimbali nchini pamoja na vyuo vya fani mbalimbali.
Taarifa iliyotolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Angelah Kairuki leo Jumapili Juni 11, 2023 amesema wanafunzi waliochaguliwa ni kutoka katika shule za serikali, binafsi, watahiniwa wa kujitegemea, waliofanya mtihani chini ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima na Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi.
Amesema, muhula wa kwanza kwa wanafunzi wa Kidato cha Tano utaanza Agosti 4, 2023  na kuwataka Wanafunzi wote waliopangwa kujiunga na Kidato cha tano kuanza kuripoti shuleni ikuanzia Agosti, 13 na mwisho ni Agosti 31 na kwamba hakutakuwa na fursa ya kufanya mabadiliko yoyote ya Shulekutokana na
ukosefu wa nafasi.
Amesema, matokeo ya mtihani wa kidato cha nne mwaka 2022 yanaonyesha kuwa watahiniwa 192,348 walipata ufaulu wa daraja la kwanza hadi la tatu ambapo kati yao Tanzania Bara walikuwa watahiniwa 188,128 wakiwemo wasichana 84,509 na wavulana 103,619.
“Matokeo ya mtihani wa kidato cha nne mwaka, 2022 yanaonesha kuwa
Watahiniwa192,348 sawa na asilimia 36.95 walipata ufaulu wa Daraja la I hadi III.
“Kati ya hao Tanzania Bara walikuwa watahiniwa 188,128  wakiwemo wasichana 84,509 na wavulana 103,619.”Amesema
Tazama hapa orodha ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano, Vyuo vya Ualimu na Vyuo vya Elimu ya Ufundi mwaka,2023 yaselform.tamisemi.go.tzna Baraza la Taifa la Elimu ya Mafunzo ya Ufundi yawww.nacte.go.tz.
Amesema, wanafunzi hawa wote wamekidhi vigezo vya kujiunga
na kidato cha tano,vyuo vya ualimu, vyuo vya elimu ya ufundi na kati kwa
mwaka,2023.
Amesema Idadi hiyo inajumuisha wanafunzi wenye mahitaji maalum 490
ambao wasichana ni 218 na wavulana ni 272.
Aidha, wanafunzi wote 188,128waliokidhi vigezo wamechaguliwa na kupangiwa
kujiunga na Kidato cha Tano katika shule mbalimbali nchinipamoja na Vyuo
vya fani mbalimbali.
 Amesema Wanafunzi 129,830 wakiwemo wasichana 66,343na wavulana 63,487 sawa na asilimia 69 ya wenye sifa, wamechaguliwa kujiunga na Shule za Sekondari za Kidato cha tano.
Akitoa mchanganuo Kairuki anasema
(Wanafunzi1,878wakiwemo wasichana 1,097na wavulana 781wamepangiwa katika Shule za sekondari Maalum  nane za Kilakala, Mzumbe, Ilboru, Kisimiri, Msalato,Kibaha, Tabora Boys na Tabora Girls.
Wanafunzi 122,908 wakiwemo wasichana 62,731 na wavulana
60,177 wamepangiwa katika shule 519za Sekondari za Bweni za Kitaifa za Kidato cha Tano.
(Wanafunzi 5,044wakiwemo wasichana 2,515na wavulana 2,529 wamepangwa katika shule11 za Sekondari za Kutwa za Kidato cha Tano.
Pia, Wanafunzi 58,298 wakiwemo wasichana 18,166na wavulana 40,132
sawa na asilimia 31wamepangiwa kujiunga kwenye kozi mbalimbali
za Stashahada katika Vyuo vya Kati vinavyosimamiwa na Baraza la
Taifa la Elimu yaUfundi (NACTVET).
Akitoa mchanganuo wake, Kairuki amesema  katika mchanganuo Wanafunzi 1,645  wakiwemo wasichana 646 na wavulana 999 wamechaguliwa kujiunga na vyuo vya Ualimu ngazi ya Stashahada ya Sayansi, Hesabu na TEHAMA.
Wanafunzi 1,877wakiwemo wasichana 757na wavulana 1,120 wamechaguliwa kujiunga na fani mbalimbali katika Vyuo  vinne vya Elimu ya Ufundi ambavyo ni Chuo cha Ufundi cha Arusha (ATC), Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Chuo Kikuu cha Sayansi na
Teknolojia Mbeya -MUST na Chuo cha Usimamizi na Maendeleo ya Maji (WDMI).
Amesema, wanafunzi 1,842 wakiwemo wasichana 943 na wavulana 899
wamechaguliwa kujiunga na vyuo vya Afya ngazi ya Stashahada.
Wanafunzi 52,934 wakiwemo wasichana 15,820na wavulana 37,114 wamechaguliwa kujiunga kwenye kozi mbalimbali zikiwemo za Kilimo, Ufugaji,Utawala, Biasharana zinginezo za Stashahada katika Vyuo vya kati mbalimbali nchini.

Habari Zifananazo

Back to top button