SERIKALI imetakiwa kutafakari upya utoaji wa leseni za biashara hasa kwa watu ambao wanaanza biashara.
Wito huo umetolewa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana, wakati akizungumza na wananchi wa Mkoa wa Kagera.
Kinana amesema kuna mambo yasiyo ya lazima, ambayo yanawekwa kwenye masharti ambayo mwisho wake huwa ni kumfilisi mtu.
“Utakuta mtu ana mtaji wa Sh 200,000, lakini anatakiwa leseni sasa atakavyozungushwa, malipo na urasimu wake utakuta sh 200,000 zimekwisha na hana pesa tena, sijui nini maana yake,” alisema Kinana.
Aliwataka wabunge kuwa ngangali wakati wa upitishaji wa sheria na kuacha kuiga maamuzi ya maofisa kwa kuwa wao wapo wakati wote.