Kinana aahidi jambo wakulima wa pamba

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)  Abdulrahman Kinana ametembelea mashamba ya pamba wilayani Itilima, mkoani Simiyu ili kujionea ustawi wa zao hilo.

Kinana amefikia hatua hiyo baada ya kupokea malalamiko  kutoka kwa wakulima wa zao hilo kuhusu  kuporomoka kwa bei.

Advertisement

Mwaka jana kilo moja iliiuzwa sh 2,000 lakini mwaka huu imeporomoka hadi sh 1,200.

Akiwa shambani hapo Kinana ameahidi kukutana na Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe, kesho mkoani Tabora na kuzungumza naye kuhusu mustakabali wa kunusuru zao hilo.

“Kesho nitakua na Bashe, nitazungumza naye kwa kina, tuangalie namna ya kuwasaidia wakulima wa pamba na kulinusuru zao hili kuporomoka,” amesisitiza.

5 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *