MICHEZO ya hatua ya 16 bora ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Ulaya (EURO 2024 inaanza kupigwa leo kwa mechi mbili.
Mabingwa watetezi Italia itatinga dimbani kukipiga dhidi ya Uswisi kwenye uwanja wa Olympia uliopo jiji la Berlin.
Mchezo wa pili utashuhudia wenyeji Ujerumani wakikiwasha dhidi ya Denmark kwenye uwanja wa Signal Iduna uliopo jiji la Dortmund.
Timu nyingine kwenye kinyang’anyiro cha 16 bora ni Slovakia, England, Hispania, Georgia, Ufaransa, Ubelgiji, Ureno, Slovenia, Romania, Uholanzi, Austria na Uturuki.