Kitayosce, Fountain Gate zafungiwa usajili

KLABU ya Kitayosce inayoshiriki ligi kuu Tanzania bara pamoja na Fountain Gate inayoshiriki ligi ya Championship zimefungiwa kusajili wachezaji kutokana na kushindwa kumlipa aliyekuwa Kocha wao.

Taaarifa iliyotolewa na shirikisho la soka Tanzania TFF leo Julai 12 imesema uamuzi huo umekuja baada ya kocha Ahmed El Faramawy Yousef kushinda kesi ya madai dhidi ya klabu hizo.

Kocha huyo raia wa Misri ambaye alizifundisha timu hizo kwa vipindi tofauti alifungua kesi FIFA akipinga kuvunjiwa mkataba kinyume cha taratibu.

Taaarifa hiyo ya TFF imesema baada ya kocha huyo kushinda kesi yake timu hizo zilipaswa kumlipa ndani ya siku 45 lakini zimeshindwa kufanya hivyo na shirikisho la soka ulimwenguni FIFA limezifungia kufanya usajili wa kimataifa huku TFF ikizifungia kufanya usajili wa ndani.

Aidha TFF wamezitaka timu mbalimbali kuzingatia vipengele vya kimkataba kabla ya kuvunja mkataba na makocha au wachezaji.

Habari Zifananazo

Back to top button