MECHI kadhaa za Ligi Kuu England(EPL), Ligi Kuu Ujerumani(Bundesliga) na Italia(Serie A) zinaendelea leo kwenye viwanja tofauti.
Liverpool inaendelea kuongoza msimamo wa EPL ikiwa na pointi 46 baada ya michezo 19 wakati Southampton ni ya 20 mwisho wa msimamo ikikusanya pointi sita.
Huko Ujerumani baada ya michezo 16, Bayern Munich inaongoza Bundesliga ikiwa na pointi 39 huku VfL Bochum ipo nafasi ya 18 mwisho msimamo ikiwa na pointi nane.
Miamba ya Jiji la Naples, Italia klabu ya Napoli ni kinara wa Serie A hadi sasa ikiwa na pointi 47 baada ya michezo 20 wakati mwisho wa msimamo wa timu 20 zinashiriki ligi hiyo ipo Monza yenye pointi 13.
Mitanange inayopigwa leo ni kama ifuatavyo:
PREMIER LEAGUE
Brentford vs Manchester City
Chelsea vs Bournemouth
West Ham United vs Fulham
Nottingham Forest vs Liverpool
BUNDESLIGA
Holstein Kiel vs Borussia Dortmund
Bayer Leverkusen vs Mainz 05
Eintracht Frankfurt vs Freiburg
Wolfsburg vs Borussia M’gladbach
SERIE A
Como 1907 vs AC Milan
Atalanta vs Juventus