Kivumbi mtoano kubaki Ligi Kuu leo

MCHEZO wa kwanza wa mtoani kuwania kubaki Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Fountain Gate na Tanzania Prisons unapigwa leo mkoani Manyara.

Mchezo huo utafanyika kwenye uwanja wa Tanzanite Kwaraa uliopo mjini Babati.

Mchezo wa marudiano utafanyika Juni 30 kwenye dimba la Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.

Tanzania Prisons imeshika nafasi ya 13 katika msimamo wa ligi hiyo iliyofikia tamati Juni 25 kwa Yanga kutetea ubingwa wakati Fountain Gate imeshika nafasi ya 14.

Kagera Sugar na KenGold zimeshuka daraja.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button