Kombe la UEFA Super kupigwa Poland leo

REAL Madrid ya Hispania na Atalanta ya Italia zinashuka dimbani leo katika mchezo kuwania Kombe la UEFA Super.

Mchezo huo utafanyika kwenye wa Taifa katika mji mkuu wa Poland, Warsaw ukiamuliwa na pilato Sandro Schaerer kutoka Uswisi.

Mechi ya Kombe la UEFA Super barani Ulaya hupigwa kabla ya Ligi za mataifa mbalimbali kuanza ikihusisha bingwa wa Ligi ya Mabingwa na Ligi ya Europa.

SOMA: UEFA yatangaza muundo mpya wa mashindano

Real Madrid na Atalanta zimekutana mara mbili pekee katika historia yao, mechi zote zikiwa katika Ligi ya Mabingwa ya UEFA msimu wa 2020-2021.

Zilikutana kwa mara ya kwanza Februari 24, 2021, katika Uwanja wa Gewiss uliopo Bergamo, Italia.

Real Madrid ilishinda kwa 1-0, bao la dakika za jionilikifungwa na Ferland Mendy.

Mchezo uliofuata akati ya timu hizo ulifanyika Machi 16, 2021, katika Uwanja wa Alfredo Di Stéfano, Madrid.

Real Madrid ilijihakikisha nafasi ya robo fainali kwa ushindi wa 3-1 dhidi ya Atalanta kwa mabao kutoka kwa Karim Benzema, Sergio Ramos, na Marco Asensio huku Luis Muriel akifunga bao la kufutia machozi kwa Atalanta.

Habari Zifananazo

Back to top button