Kundi la Houthi lakiri kushambulia Tel Aviv

Shemu ya moja ya majengo yaliathiriwa na shmbulio la kundi wa Houthi la Yemen katika jiji la Tel Aviv, Israel.

KUNDI la waasi wa Houthi la Yemen limekiri kuhusika katika shambulio la ndege isiyo na rubani leo karibu na Ubalozi wa Marekani katikati ya Tel Aviv, Israel na kusababisha kifo cha mtu mmoja na kujeruhi wengine 10.

Shambulio hilo la anga limetikisa mitaa na kusababisha vipande vya mlipuko kuanguka na kusambaza vipande vya kioo katika eneo kubwa.

Waasi wa kihouthi wamekuwa wakirusha ndege zisizokuwa na rubani na makombora kuelekea Israeli wakati wote wa vita vya Israel na Hamas kuunga mkono watu wa Palestina dhidi ya Israel.

Advertisement

SOMA: Mashambulizi ya Israel yanateketeza familia Gaza

Msemaji wa Houthi, Yahya Sare’e amesema katika taarifa iliyochapishwa kwenye mitandao wa X kwamba shambui hilo limefanywa kulipiza kissi ya vita hiyo na limepiga moja ya malengo mengi ya kundi hilo.

Kundi hilo la Houthi limedai kwamba ndege zao mpya zisizo na rubani zinaweza kupita mifumo ya ulinzi wa anga ya Israeli.

Afisa wa kijeshi wa Israel ambaye hajatajwa jina amesema tathmini ya jeshi kuhusu vitisho vya angani haijabadilika kwa sababuingawa maadui wa wa nchi hiyo wamejaribu mikakati hiyo kwa miezi kadhaa.

“Lilikuwa ni shambulio la kigaidi lililolenga kuua raia nchini Israel,” ameeleza afisa huyo kuhusu shambulio hilo la kwanza kutishia Tel Aviv kwa miezi mingi.

Kamanda wa Wilaya ya Tel Aviv, Peretz Amar, amesema maafisa hawakuweza kubaini mahali pa shamblio wakidai kwamba mlipuko ulitokea angani; hata hivyo, jeshi la Israel limesema halikutambua iwapo ni ndege isiyo na rubani au vipande vyake vimepiga majengo.

Shambulio hilo lilihariiu madirisha ya majengo na magari kadhaa katika eneo la karibu na pwani.

Wengi wa raia Elfu-60 wa Israel waliohamishwa kutoka kwenye nyumbani zao mwazo wa vita kati ya nchini hiyo na Hamas walijikuta wakiweka makazi eneo hilo

Shambulio la Wahouthi limekuja saa chache baada ya jeshi la Israel kuthibitisha kwamba moja ya mashambulizi yake ya angani yalikuwa yameua kamanda wa Hezbollah na wapiganaji wengine Kusini mwa Lebanon.