Waasi M23 waanza safari ya Butembo

DR CONGO: WAASI wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda wameonekana kuelekea mji wa Butembo, Mashariki mwa DR Congo, ambapo mapigano makali yameonekana kwenye barabara zinazoelekea mji huo.

Mashuhuda na wakazi wa eneo hilo wamesema hali inaendelea kuwa mbaya, na taarifa hiyo imethibitishwa na Auguste Kombi, kiongozi wa shirika la kiraia la Kitsombiro.

Katika hali hiyo, msemaji wa jeshi la Uganda, Felix Kulayigye, amesema kuwa kwa makubaliano na serikali ya Kinshasa, Uganda imewatuma wanajeshi wake katika mji wa Bunia, mashariki mwa DR Congo, kukabiliana na wanamgambo wa eneo hilo na kuokoa maisha ya raia.

Bunia ni mji mkuu wa jimbo la Ituri, ambapo Uganda ina maelfu ya wanajeshi wakiunga mkono vikosi vya DR Congo katika vita dhidi ya waasi wa ADF. SOMA: AU yahofia mgawanyiko DR Congo

Kwa sasa  mji wa Butembo una idadi ya watu wasiopungua 150,000, takriban kilometa 210 Kaskazini mwa Goma.

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button