Kuondoa adha ya mafuriko Simanjiro

Mafundi wakiendelea na ujenzi wa moja ya makalavati yaliyopo katika Barabara ya Moshi-Simanjiro, Kata ya Msitu wa Tembo wilayani Simanjiro, Mkoa wa Manyara ambalo ni miongoni mwa miradi inayotekelezwa na Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA). Kukamilika kwa daraja hilo na mengine kutaondoa adha ya mafuriko kwa wananchi wa eneo hilo ambayo yamekuwa yakizorotesha shughuli za uchumi. (Picha na Fadhili Akida).