ENGLAND: MENEJA wa Manchester United, Erik ten Hag amesema anahisi “sio haki na dhuluma” baada ya mwamuzi, David Coote wa mchezo dhidi ya West Ham United kukubali penalti ya dakika za mwisho jana.
Beki wa United, Matthijs de Ligt alimfanyia madhambi mshambuliaji wa West Ham, Danny Ings eneo la hatari, baada ya majadiliano na waamuzi wa chumba cha VAR, Coote aliamua kujiridhisha kupitia usaidizi wa video na kuamua penalty.
SOMA: Manchester United haijamsahau Frenkie de Jong
“Nilizungumza nao,” alisema Ten Hag. “Lakini uamuzi umeshafanywa. Hakuna njia nyingine na hilo ni soka.
“Hii ni mara ya tatu tunakosa haki msimu huu na ina athari kubwa kwa timu yetu na kwa alama zetu na mahali tulipo kwenye msimamo sio sawa” amesema Ten Hag.
Win, lose or draw — we hear you every game, Reds.
Thanks for your magnificent support on the road once again 🔴#MUFC || #WHUMUN pic.twitter.com/KsAoOBXTJn
— Manchester United (@ManUtd) October 27, 2024