Kweweta ajitosa ubunge Kilwa Kusini

KILWA: KATIBU Mkuu Kiongozi wa Baraza Kivuli la Mawaziri wa ACT Wazalendo, Idrisa Kweweta amechukua rasmi fomu ya kugombea Ubunge wa Jimbo la Kilwa Kusini kupitia tiketi ya chama hicho.
Fomu hiyo alikabidhiwa na Katibu wa Jimbo, Twahir Bingwe, mbele ya wanachama, viongozi wa chama, na wananchi waliokusanyika ofisi za jimbo hilo.
“Lengo langu ni kurejesha heshima ya Kilwa, heshima ya maendeleo, heshima ya sauti ya wananchi, na heshima ya utawala wa haki,” amesema Kweweta.
SOMA ZAIDI: ACT yaongeza muda kuchukua, kurejesha fomu uchaguzi …
Mbali na dhamira hiyo, Kweweta aligusia changamoto kubwa zinazoikumba Kilwa Kusini ikiwemo ubovu wa miundombinu ya barabara, huduma duni za afya, na mfumo dhaifu wa elimu na kuwa endapo atapata ridhaa ya kuongoza atashughulikia changamoto hizo.