‘Maadili ni msingi uongozi bora’

MOROGORO: OFISI ya Rais ,Sekretarieti ya Maasili ya viongozi wa Umma imewataka viongozi kuzingatia misingi ya maadili kwenye utumishi wao kwani huimarisha imani ya wananchi kwa Serikali na taasisi zake kitendo kinachoongeza ushirikiano, utiifu wa sheria na mshikamano wa jamii.

Kamishna wa Maadili katika Ofisi hiyo, Jaji Mstaafu, Sivangilwa Mwangesi amesema  hayo kupitia hotuba ya ufunguzi wa mafunzo ya maadili kwa viongozi wa umma  ilisomwa kwa niaba yake na Kamishna , Ofisi ya Rais , Tume ya  Utumishi wa Umma ,Nassor Mnambila, mjini Morogoro.

Mnambila pia ni kiongozi wa wawezeshaji  wa mafunzo yaliwashirikisha mameya ,wenyeviti wa halmashauri, wakurugenzi watendaji pamoja na wajumbe wa madiwani wa kamati za maadili za mabaraza ya halmashauri mbalimbali nchini.

Jaji Mstaafu Mwangesi amesema maadili si suala la hiari bali ni msingi wa uongozi bora, hivyo viongozi wa umma wanatakiwa kuwa kielelezo cha uaminifu, uwazi, usawa na uzingatiaji wa sheria katika maamuzi yao ya kila siku.

Amesema kulingana na mazingira ya sasa ya utumishi wa umma, mafunzo ya maadili kwa viongozi ni suala muhimu ,hasa katika kipindi ambazo kuna mtanziko mkubwa wa changamoto za kimaadili kuanzia ngazi ya familia, jamii na taifa kwa ujumla.

Jaji Mstaafu Mwangesi amesema maadili husaidia kuzuia migongano ya maslahi , matumizi mabaya ya madaraka, rushwa , upendeleo na hujenga utamaduni wa uwajibikaji, huimarisha nidhamu ya kiutumishi na huongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya umma.

“Maadili ni kinga ya maovu yote na nguzo muhimu ya utawala bora na maendeleo endelevu wa taifa nah ii kutokana na mitizamo ya  jamii inavyowachukulia vongozi wao hawatimizi wajibu wao kwao,“ amesema Jaji Mstaafu kupitia hotuba yake hiyo.

Naye Katibu Msaidizi, Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Kanda ya Kaskazini, Gerald Mwaitebele amesema ofisi hiyo na Chuo cha Uhasibu Arusha zimeingia makubaliano ya kushirikiana katika maeneo ya  kutoa mafunzo ya maadili na utawala bora kwa viongozi wa umma.

Mwaitebele ambaye pia ni Mratibu wa Mafunzo hayo, ametaja eneo lingine ni kutoa ushauri kuhusu masuala yahusuyo maadili na kufanya utafiti kuhusu masuala yahusuyo maadili.

Amesema  mafunzo hayo ya awamu ya pili yataendelea kuanzia Aprili hadi kufikia Juni, 2026 kwa makundi tofauti ya viongozi mbalimbali watakaoshiriki kwenye vituo watakavyochangua ambayo ni Morogoro, Mwanza na Arusha.

Kwa upande wake Meya wa Manispaa ya Tabora, GulamHussein Dewji ambaye amekuwa miongoni mwa washiriki amesema mafunzo hayo yatawajengea  uwezo kuwa na maadili mema kwenye uongozi wanaoutumikia kwa wananchi .

“Kikubwa mafunzo hayo yakizingatiwana wote ,nchi yetu itabadirika , kwani  kiongozi anayefuata maadili kwenye taasisi yake , mabadiliko lazima yawepo kutokana kujengewa uwezo  huo na kufanya taasisi watakazo ziongoza zitakuwa na uweledi” amesema Meya Dewji.

Habari Zifananazo

3 Comments

  1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 12000-16700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
    .
    This is my main concern…………………… http://Www.Cash54.Com

  2. I just came across this amazing way to earn $11,000-$15,000 a month online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
    .
    This is what I do…………………… http://Www.Payathome9.Com

  3. JOIN US The finest part-time income opportunity to work on mobile or laptop earn more than $300💵 every day. In the preceding month, I earned $11,683💵 by working 3 or 4 hours every day online.

    Simply visit this website for further information………………… https://Www.PayAtHome1.Com/

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button