LIBERIA : RAIS wa Liberia, Joseph Boakai, amewaondoa kazini zaidi ya maafisa 450 wa serikali kwa kushindwa kutangaza mali zao kama ilivyoelezwa na sheria za nchi.
Tume ya Kupambana na Ufisadi ya Liberia (LACC) ilibaini kuwa maafisa 457, wakiwemo Waziri wa Bajeti na mabalozi, hawakufanya tangazo la mali zao kabla ya tarehe ya mwisho ya Novemba, kinyume na kanuni za maadili za serikali.
Ofisi ya Rais ilisema kuwa maafisa hao watasimamishwa kazi kwa mwezi mmoja bila malipo hadi watakapowasilisha nyaraka zinazohitajika.
Sheria ya Liberia inawataka watumishi wa umma kutangaza mali zao wanapoingia au kuondoka katika nyadhifa zao ili kuhakikisha uwazi na kuepuka ufisadi serikalini. SOMA: Wafuasi watatu wa Rais mteule Liberia wafa