WATU* watatu wamekufa na wengine 20 wako hospitalini nchini Liberia baada ya gari kuwagonga wafuasi wa Rais mteule, Joseph Boakai, Ofisa Afya ameeleza.
–
Imeripotiwa baada ya mkasa huo, dereva alilitelekeza gari hilo katika eneo karibia na ofisi za chama.
–
Polisi wameanzisha msako, hata hivyo gari hilo lilichomwa moto na wananchi walioshuhudia tukio hilo.
–
Juamatatu jioni wafuasi wa Boakai walisherehekea tangazo rasmi la ushindi nje ya Makao Makuu ya Chama cha Unity Party (UP) mji Mkuu wa Monrovia.
–
Polisi walitaja tukio hilo kama ajali, hata hivyo UP ilisema tukio hilo lakigaidi.
–
Home Wafuasi watatu wa Rais mteule Liberia wafa
Comments are closed.