Mabaharia Tanzania kutambulika zaidi kimataifa

SERIKALI kupitia Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), imeendelea na juhudi za kuwafungulia fursa mabaharia wa Tanzania kimataifa.

Kwa niaba ya Serikali TASAC ilisaini Hati ya Makubaliano (MOU) na nchi ya Barbados ili nchi hizo mbili ziweze kutambua vyeti vya mabaharia wa kila upande. Tanzania kwa sasa imesajili vyeti 17,689 vya mabaharia.

Akizungumza mara baada ya kusainiwa kwa makubaliano hayo  jijini London, Uingereza, Mkurugenzi Mkuu wa TASAC ambaye pia ni Msajili wa Mabaharia na Meli nchini, Bw. Kaimu Abdi Mkeyenge amesema hadi sasa Tanzania imeanzisha mawasiliano na majadiliano na Nchi 34 kwa ajili ya kuingia katika makubaliano ya kutambulika kwa vyeti vya Mabaharia wa pande hizo.

Alisema hatua hiyo ni fursa nzuri ya ajira za kimataifa kwa mabaharia wa Tanzania, lakini pia itasaidia kuondoa usumbufu wa kushushwa kwa mabaharia wa kitanzania katika meli mbalimbali ambazo zimesajiliwa na nchi ambazo Tanzania haina mkataba nazo.

Barbados ni nchi ya Kisiwani katika Bahari ya Karibi takriban kilomita 430 Kaskazini-Mashariki mwa Venezuela, mpaka sasa ina usajili wa wazi na masharti nafuu (open registry) wa meli 400.

Nchi jirani za karibu kuvukia bahari ni Saint Lucia na Saint Vincent upande wa Magharibi, Trinidad na Tobago upande wa Kusini na Grenada upande wa Kusini-Magharibi.

Nchi nyingine ambazo Tanzania imeshaanzisha mawasiliano na majadiliano ni pamoja na Bahamas, Algeria, Korea ya Kusini, China, Comoros, Cyprus, Misri, Ufaransa, Ghana, India, Iran, Kenya, Liberia, Malta, Marshall Islands, Mongolia, Oman, Palau, Panama, Peru, Qatar, Saudi Arabia, Singapore, Africa Kusini, Shelisheli, Uturuki, Umoja wa Falme za Kiarabu, Vanuatu, Vietnam na nchi za Umoja wa Ulaya.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Julia
Julia
1 month ago

Making an extra $15,000 per month from home by performing simple internet copy and paste jobs. This basic at-home job paid me $18,000 each year. Everyone may now easily make extra money online.
.
.
Detail Here————————————————————>>>  http://Www.BizWork1.Com

Ruth T. Medina
Ruth T. Medina
1 month ago

I’ve gained only within four weeks by comfortably working part-time from home. Immediately when I had lost my last business, mtg I was very troubled and thankfully
following website___________ http://Www.Careers12.com

Last edited 1 month ago by Ruth T. Medina
Back to top button
2
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x