Mabalozi wawapongeza Samia, Nchimbi

Mgombea wa urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi CCM katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu, Samia Suluhu Hassan.

JUMUIYA ya kimataifa imepongeza uteuzi wa Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea wa urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu.

Mgombea mwenza wa urais, Dk Emmanuel John Nchimbi.

Pia mabalozi wa Uganda, Algeria, India na Marekani waliopo Tanzania wamempongeza, Dk Emmanuel John Nchimbi kwa kuteuliwa kuwa mgombea mwenza wa urais na Dk Hussein Mwinyi kwa kuthibitishwa kuwa mgombea
wa urais wa Zanzibar.

Walitoa pongezi hizo wakati wa mazungumzo na Katibu Mkuu wa CCM, Dk Nchimbi kwa nyakati tofauti katika ofisi ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam.

Advertisement

Balozi wa Algeria nchini, Ahmed Djellal na wa India nchini, Bishwadip Dey waliwapongeza Rais Samia, Dk Mwinyi na Dk Nchimbi kwa kuaminiwa kupeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi huo ujao.

Naibu Balozi wa Marekani nchini, Andrew Lentz aliwatakia kila la heri viongozi hao katika uchaguzi.

Balozi wa Uganda nchini, Kanali mstaafu Fred Mwe sigye alifikisha salamu za pongezi kutoka kwa Serikali ya Uganda na chama tawala cha NRM akieleza kuwa Uganda inatambua na kuheshimu mchango wa Tanzania na CCM
katika harakati za ukombozi wa Afrika.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *