Madaktari Marekani watoa matibabu bure Moro

MOROGORO: MADAKTARI Bingwa kutoka Marekani waliopo katika Taasisi ya Global Health Humanity First inayomilikiwa na Jumuiya ya Ahamadiyya Duniani wameweka kambi ya ya utoaji  huduma za upimaji wa afya na utoaji wa matibabu bure kwa wananchi wa Manispaa ya Morogoro.

Mwenyekiti wa Taasisi, Abdulrahman Mohammed amesema hayo kwenye zoezi la utoaji wa huduma hizo katika kambi iliyowekwa katika Shule ya Msingi ya Ahamadiyya eneo la Kihonda Maghorofani kwenye manispaa hiyo.

Amesemataasisi hiyo iliyopo  chini ya Jumuiya ya Waislamu Ahamadiyya Duniani ipo kwa ajili ya huduma za kibinadamu kwenye jamii ambazo ni pamoja na afya, maji , elimu na nyinginezo.

Mwenyekiti wa Humanity first Tanzania  amesema kambi hiyo inaongozwa na madaktari kutoka vyuo vikuu vya Marekani wakiambatana na wanafunzi wa udaktari ili kutoa huduma ya upimaji wa afya na matibabu kwa wagonjwa kwa kushirikiana na madaktari bingwa wa hapa nchini hususani kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili , Dar es Salaam.

SOMA ZAIDI: MOI kutoa matibabu bure siku saba Mbagala – HabariLeo

Naye Daktari Naeem Lughman anayesimamia Idara ya Humanity First ambaye pia ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Tiba cha Toledo nchini Marekani amesema  safari hii wamekuja Tanzania wakiambatana na wanafunzi wa udaktari ili waelewe zaidi utaratibu wa matibabu duniani.

“Kwa kipindi hiki cha Mei mwaka huu 2025 tumeamua kuja nchi Tanzania na hii ni mara ya kwanza” amesema Dk Lughman.

Naye Dk Kaleem Malik wa Idara ya Majanga kwa ujumla  amesema  wamekuwa wakifanya shughuli ya kujitolea za kutoa huduma za afya kwa muda wa miaka 30 sasa.

Dk Malik amesema lengo na madhumuni ya kuja na wanafunzi wao wa udaktari ni kushirikiana na madaktari bingwa wa Tanzania wakiwa na lengo kubwa la kujitolea katika huduma za afya.

SOMA ZAIDI: Tanzania kimbilio matibabu ya kibingwa kitaifa, kimataifa

“Kujitolea kwetu ni kuzalisha fikra na uelewa ndani ya vichwa vya madaktari ya kwamba shughuli ya kutibu binadamu sio shughuli ya biashara , bali ni shughuli ya kutoa huduma kwa mwanadamu na kujitoa kabisa,” amesema Dk Malik.

Dk Malik amesema kuwa huo ndio utaratibu wa madaktari na wanafunzi wao udaktari kujitolea bure kuhudumia wananchi na hakuna anayelipwa katika shughuli zote za Humanity First.

“Moyo huu ndio ambao tunautaka tuuzalishe kwa madaktari wote na wanafunzi wa udaktari watambue kwamba ni watoa huduma kwa binadamu “ amesema Dk Malik.

“Madaktari tusimame sote tuwasaidie binadamu wenzetu bila kujali dini, ukabila ,rangi kama ni mtu Mmarekani, Mtanzania kama ni Mwafrika ,kwanza madaktari tufikirie kumhudumia mwanadamu kabla ya kufikiria kupata kitu chochote kutoka kwao, “amesisitiza Dk Malik.

Naye Naibu Amiri wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya Tanzania na Mratibu wa Humanity first nchini,Sheikh Abid Mahmood Bhatti amesema  huduma ya upimaji wa afya na utoaji wa matibabu ya afya bure ulianza Mei 18  hadi 20, mwaka huu.

Sheikh Bhatti amesema lengo ni kuwafikia wananchi wapatao 1,500 ambapo wamelenga kuhudumia watu 500 kwa siku  na hivyo kuwaomba wananchi wajitokeze kufika kupata huduma za afya bila gharama yoyote.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button