Madiwani washauri serikali kufufua viwanda vya pamba

MADIWANI wa Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama mkoani Shinyanga wameishauri serikali kufufua viwanda vya ununuaji wa zao la pamba ili kunusuru maisha ya wakulima na halmashauri kupata ushuru kupitia zao hilo.

Diwani wa kata ya Kinamapula, Sharifu Samweli amesema hayo leo kwenye kikao cha kawaida cha Baraza la Madiwani cha robo ya nne ya mwaka baada ya Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi, Uenzi na Mazingira kudai halmashauri hiyo inategemea hasa kilimo kukuza uchumi.

Diwani Samweli amesema ushauri uliopo ni aerikali kufufua viwanda vya pamba ili wakulima wanufaike wamepungua kulima zao hilo sababu ya bei kutoeleweka vizuri inapanda wakati mwingine inashuka.

“Mfano mwaka huu wakulima wameuza kwa sh 1060 kwa kilo na mwaka jana wameuza sh 2020 kwa kilo ukiuliza sababu soko la nje limeshuka lakini ningekuwepo kiwanda hapa nchini changamoto hiyo isingekuwepo.” alisema Samweli.

Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Gaga Lala amesema ushauri huo waliuongelea kwenye vikao na katibu tawala mkoa hivyo baraza litaendelea kutoa ushauri ili wakulima waweze kunufaika.

Aidha Halmashauri ya Ushetu Ina jumla ya hekta 9,167 za kilimo na wakulima 8316 ambapo mpaka Agosti 15 mwaka huu wamevuna kilogramu 3,659,790.

Habari Zifananazo

Back to top button