Mageuzi yaja sekta ya afya
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema serikali imekuwa ikitekeleza mikakati mbalimbali kuhakikisha huduma bora zinapatikana kwa watoto wachanga na mama wajawazito hivyo hatua hizo zinazochukuliwa na serikali zinaleta mageuzi makubwa ambapo kuna uwekezaji mkubwa wa huduma za afya hapa nchini.
Majaliwa amesema hivi sasa huduma maalumu za watoto wachanga (Mama Kangaroo) hadi kufikia Julai 2024 zitaanzishwa katika hospitali 245 huku kazi ya kuendeleza kuanzisha katika Hospitali nyingine zinaendelea na malengo yakiwa kila hospitali kuwa na huduma ya Mama Kangaroo.
Hayo ameyesema leo Septemba 7 Jijini Dar es salaam aliposhiriki mbio za hisani za Maendeleo Benki zenye lengo kukusanya Sh milioni 200 kusaidia watoto wanaozaliwa kabla ya wakati Hospitali ya KCMC na kituo cha watoto wenye usonji Mtoni Diaconia kitakachojengwa Bagamoyo mkoani Pwani.
WAZIRI MKUU ASHIRIKI MBIO ZA HISANI ZA MAENDELEO BANK
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Septemba 07, 2024 ameshiriki katika mbio za hisani za Maendeleo Bank Marathon 2024.
Bofya link kusoma zaidi 👇🏿https://t.co/S7xjDPXWii pic.twitter.com/ot6CsIf4PY
— Ofisi ya Waziri Mkuu (@TZWaziriMkuu) September 7, 2024
SOMA: Waziri Mkuu: Serikali imeimarisha nguvu kazi ya afya
Majaliwa amesema watoto hao wanaozaliwa kabla ya wakati wanastahili kuishi hivyo mchango wa walioshiriki mbio hizo utaenda kuokoa maisha yao ili wachangie shughuli za maendeleo ya taifa.
Majaliwa amesema Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro KCMC idadi ya vifo vya watoto wanaozaliwa kabla ya wakati ni kubwa ipo kati ya asilimia 20 mpaka 25 hivyo wanahitaji msaada na uangalizi wakutosha kwa jamii.
Kwa upande wake Msaidizi wa Askofu KKKT-Dayosisi ya Mashariki na Pwani Dean Chediel Lwiza amesema fedha hizo zote zilizopatikana zitawahudumia watoto wanaozaliwa nje ya wakati katika Hospitali ya KCMC na kituo cha watoto Diaconia.
SOMA: Ummy awaita wadau sekta ya afya
Amesema kituo cha Diaconia kilichopo kwa Azizi Ally Dar es salaam ardhi yake imevamiwa na wananchi hivyo kanisa limetoa eneo la Kitopweni Bagamoyo lenye takribani hekari 20 ili kiwezwe kujengwa kituo kikubwa cha kisasa na chenye hadhi ya Kimataifa.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo Benki, Peter Tarimo amesema ni mara ya pili benki hiyo inaandaa mbio za hisani ambapo mbio za kwanza walizofanya mwaka jana waliweza kupata Sh milioni 120 ambapo sehemu ya fedha hizo milioni 60 zilipelekwa Hospitali ya KCMC kwenye hodi ya watoto wanazaliwa kabla ya wakati na Sh milioni 60 nyingine ilielekezwa kwenye watoto wenye ulemavu wa akili na usonji kituo cha Mtoni Diakonia.
Mbio hizo za hisani Maendeleo Benki Marathoni 2024 zimebebwa na kauli mbiu ya Hatua ni faraja msimu wa pili mbio hizo zimehusisha Mbio za Kilomita .2.5 mbio za kilomita 5, Kilomita 10, na Kilomita 21.