Maghembe aahidi maji ya uhakika Ugweno

MWANGA : MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Mwanga mkoani Kilimanjaro kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Ngwaru Maghembe amesema akichaguliwa kipaumbele chake cha kwanza ni kuhakikisha wananchi wa tarafa ya Ugweno wanapata maji ya uhakika. Dk Maghembe alitoa ahadi hiyo mwishoni mwa wiki kwenye uwanja wa VTC ulioko Usangi, wilayani humo.

Wakati wa uzinduzi wa kampeni za CCM, Alisema afya ni jambo la kwanza la kuzingatiwa kwa vile watu wakiwa na afya njema wanapata fursa ya kufanya shughuli za kimaendeleo kwa manufaa yao binafsi na ya taifa kwa ujumla.

“Kwa mtu kuwa na afya njema ni pamoja na yeye kuwa na uhakika wa kupata maji safi na salama; hili naliwekea msisitizo litalifanyia kazi kwa haraka,” alisema Dk Maghembe. Kuhusu nishati ya umeme, Dk Maghembe alisema atafuatilia kuhakikisha vitongoji sita ambavyo havijapata umeme vinapata kwa muda uliowekwa.

Akizungumzia changamoto ya uvamizi wa wanyamapori ambao wamekuwa kero kwa baadhi ya wananchi wilayani Mwanga, Dk Maghembe alisema kuwa ataandaa mpango utakaowezesha kukabiliana na changamoto hiyo kwa ukaribu zaidi. SOMA: Ruwasa yaokoa maisha ya watu 6,300 Inyara

“Nitashirikiana na mamlaka husika kuhakikisha TAWA inafungua ofisi yake wilayani Mwanga ili kuwepo na maofisa wa taasisi hiyo kwa karibu pale watakapohitajika haraka tofauti na sasa ambapo wanalazimika kusafiri kutoka wilaya ya Same pale wanapohitajika,” alisema Maghembe. Kuhusu malipo ya fidia kwa ambao wameathirika na uvamizi wa wanyamapori, mgombea huyo alisema kuwa atafuatilia suala hilo mapema iwezekanavyo baada ya kubainika kwamba mara ya mwisho kwa watu kulipwa fidia hiyo ni mwaka wa 2022.

Aidha, alisema kiapumbele kingine ni kuhakikisha wananchi wa kata za Msangeni, Kivisini, Mwaniko, Chomvu, Ngujini na Kirya wanapata mawasiliano ya uhakika. Dk Maghembe alisema atashirikiana na mamlaka husika wilayani Mwanga kuhakikisha vijana wanapata elimu bora ya ujasiriamali sambamba na kuhakikisha mikopo ya halmashauri kwa upande wa vijana inaboreshwa na kupatikana kwa wakati ili waweze kujiajiri badala ya kungoja kuajiriwa baada ya kuhitimu masomo yao.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button