WAZIRI Mkuu, Kassim Majal iwa ameiagiza Kamati ya Wataalamu ya Uchunguzi wa jengo lili loporomoka katika eneo la Kariakoo ifanye kazi kwa weledi.
Majaliwa alisema hayo kwenye Ofisi Ndogo ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es Salaam wakati anaizindua kamati hiyo kutekeleza maagizo ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuchunguza chanzo cha tukio hilo pamoja na kufahamu ubora na uimara wa majengo yote yaliyoko Kariakoo.
Ameiagiza ifanye uchun guzi wa kina, kwa uwazi, haki na kwa kuzingatia viwango vya kitaaluma.
“Taifa limewatuma nen deni mkaifanye kazi hii na mlete matokeo,” alisema Ma jaliwa na akaitaka itekeleze majukumu yake kwa kufuata sheria, kanuni na maadili ya kazi.
Soma pia:Vifo vyafikia 20 Kariakoo
Alisema kamati hiyo itachunguza jengo hilo lililo poromoka, majengo mengine yanayoendelea kutumika katika eneo la Kariakoo na pia itachunguza uimara wa majengo yanayojengwa.
Majaliwa alisema pia itac hunguza endapo taratibu zin azingatiwa wakati wa ujenzi ikiwemo vibali, wakandarasi wenye sifa na usimamizi wa mamlaka husika wakati wa ujenzi.
Alisema pia kamati hiyo imeundwa ichunguze endapo uboreshaji wa majengo unao fanywa Kariakoo unazingatia sheria, kanuni na taratibu na kubainisha majengo yote yaliyo katika hatari ya kuan guka na kupendekeza hatua za kuchukua.
Novemba 16, mwaka huu saa 3 asubuhi jengo la ghorofa liliporomoka katika mtaa wa Agrey Kata ya Kariakoo mkoani Dar es Salaam na kusababisha vifo vya watu 20.
Timu ya uokoaji jana ilianza kutumia mitambo kufukua mabaki ya jengo hilo na kukusanya vifusi.
Wakati hayo yakiendelea askari kutoka vyombo vya ulinzi na usalama walishiriki kutoa mizigo zikiwemo nguo zilizokuwa zimefukiwa katika vifusi hivyo.
Pia, huduma za kijamii zimeendelea kutokelewa kwa timu ya uokoaji vikiwemo vyakula, vinywaji na taa zili fungwa kwa ajili ya kuende lea na kazi usiku.