Majaliwa: Fanyeni biashara kwa kujiamini, weledi

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa, amewataka wafanyabiashara kufanya shughuli zao kwa kujiamini, weledi na uzalendo huku wakizingatia kanuni, sheria na taratibu zilizowekwa sambamba na utamaduni wa kitanzania.

Kauli hiyo ameitoa leo Julai 5, 2023 katika hotuba yake ya ufunguzi rasmi wa Maonesho ya Kimataifa ya 47 ya biashara nchini, Sabasaba 2023, Dar es Salaam.

Advertisement

“Kama msemo wa wahenga unaosema chema chajiuza, tangazeni biashara zenu kupitia vyombo vyetu vya habari, tunazo televisheni nyingi na zile za mifumo ya online zipo tangazeni biashara zenu na huo ndio utamaduni na utaratibu wa kutangaza biashara zenu ndani na nje ya nchi, na hili ni la muhimu san,” amesema.

Amewataka wafanyabiashara wawe huru kwa yeyote mwenye maoni yenye tija na maslahi kwa taifa asisite kuifikisha kwenye mamlaka mbalimbali, huku akisisitiza kuwa milango ya serikali ipo wazi kuyasikiliza na kuyashughulikia.

“Na hapa uwanjani pale kwenye jengo la Tantrade wanapokea maoni ya wadau wetu, wafanyabiashara na yeyote mwenye wazo la maboresho ya eneo letu tutayapokea na kuyafanyia kazi,” amesema.

Kwa upande mwingine amechukua fursa hiyo kuwataka wafanyabiashara nchini kuhakikisha miamala ya kibiashara wanayoifanya wawe wanatoa na kupokea risiti.

3 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *