Majaliwa kukagua, kuweka jiwe msingi shule Mwanza

MAPOKEZI ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika uwanja wa ndege wa Mwanza leo.
Anatarajiwa kukagua na kuweka jiwe la msingi katika shule ya Sayansi ya Wasichana Mwanza iliyopo Kisesa wilaya ya Magu.
Majaliwa amepokelewa na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Mwanza na mawaziri akiwemo Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Zainab Katimba.