Majaliwa: Njooni muwekeze sekta ya utalii

Majaliwa: Njooni muwekeze sekta ya utalii

WAZIRI Mkuu, Kassimu Majaliwa amewashauri wawekezaji kuja kuwekeza nchini kwenye sekta ya utalii, kwa sababu ya amani na  utulivu na kwamba Watanzania ni  watu wenye ukarimu.

Pia amepongeza uamuzi wa Katibu Mkuu Mtendaji wa Shirika la Utalii Duniani (UNWTO), Zurab Pololikashvili na washiriki wake kuungana  na Tanzania katika  jitihada za kutunza mazingira kwa  kupanda miti baada ya mkutano huo

Akizungumza leo jijini Arusha kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan,  wakati akifungua mkutano wa 65 wa UNWTO, Kamisheni ya Afrika, Waziri Mkuu Majaliwa, alisema Tanzania licha ya amani na utulivu pia ina maeneo mengi ya uwekezaji.

Advertisement

/* */