Makamu wa Rais amjulia hali Dugange

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip  Mpango amemjulia hali  Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Dkt. Festo Dugange leo  Aprili 29, 2023 wakati alipofika hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Benjamin Mkapa baada ya kupata ajali ya gari.

Taarifa ya Tamisemi iliyotolewa leo inasema kuwa Dkt. Dugange alipata ajali usiku wa  Aprili 26, 2023 wakati akiendesha gari yake binafsi Jijini Dodoma ambapo kwa sasa anaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Benjamini Mkapa.

Advertisement

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *