Makundi maalumu kujiunga NeST maombi ya zabuni

ARUSHA: TAASISI za ununuzi zimeagizwa kutenga asilimia 30 za ununuzi wa mwaka kwa ajili ya kampuni za wazawa na makundi maalum ili kuhakikisha zabuni zilizotengwa zinatolewa kwa wazawa kwaal ajili ya ukuaji wa uchumi jumuishi
Aidha, halmashauri zote nchini zimeagizwa kuunda vikundi maalum vya vijana, walemavu ,wanawake na wazee katika maeneo yao ili viweze kujiunga na mfumo wa NeST katika maombi ya zabuni mbalimbali za serikali.
Hayo yamesemwa jijini Arusha na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dk Dorothy Gwajima kwa niaba ya Waziri wa Fedha Dk Mwigulu Nchemba wakati wa ufunguzi wa Kongamano la 9 la Ununuzi wa Umma la Mwaka 2025,lenye kauli mbiu ya Ununuzi wa Umma Kigiditali kwa Maendeleo Endelevu, Ukuzaji wa Kampuni na Makundi maalum kwa Ukuzaji wa Kampuni za Wazawa na Makundi Maalum kwa Ukuaji wa Uchumi Jumuishi
Dk Gwajima amesema endapo taasisi hizo zikitoa zabuni kwa mwaka wazawa yakiwemo makundi maalum wanawake na vijana yatawezesha sekta ya ununuzi kukua zaidi na kusisitiza taasisi hizo za nunuzi zisimamie utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa ufanisi zaidi
Naye, Mkurugenzi Mkuu wa PPRA, Dennis Simba amesema washiriki zaidi ya 1500 wanashiriki kongamano hilo huku jumla ya wazabuni 38,163 waliidhinishwa na kusajiliwa kati ya hao 36,377 ni wazabuni wa ndani na 1,786 ni wazabuni kutoka nje ya nchi.
Amesema pia taasisi za ununuzi 61,415 zikiwemo taasisi kuu ngazi za chini za serikali za mitaa zimesajiliwa na NeST ambapo miongoni mwa taasisi hizo kunataasisi kuu na kasimiwa 1,701.