Mambo yameiva Mkutano Mkuu TOC

MKUTANO Mkuu wa mwaka wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) unafanyika kesho mjini Morogoro na maandalizi yamekamilika.

Katibu Mkuu wa TOC, Filbert Bayi amesema kuwa mkutano huo ni wa kawaida na utajadili mambo mbalimbali, ikiwemo taarifa ya Katibu Mkuu, taarifa ya mwaka na maandalizi ya Michezo ya 23 ya Olimpiki itakayofanyika Paris 2024.

Bayi alisema kuwa kila kitu kimekamilika kwa ajili ya mkutano huo na tayari viongozi kutoka vyama na mashirikisho ya michezo Tanzania Bara na Zanzibar wameshaanza kuwasili mjini hapa kwa ajili ya mkutano huo.

Wakati huohuo, Mkutano Mkuu wa Kamisheni ya Wachezaji ulifanyika jana na kujadili mambo mbalimbali, na kubwa kuvisisitizia vyama kuendesha mashindano yao ya taifa na kuundwa kwa Kamisheni za Wachezaji katika vyama vyao.

Jumla ya washiriki 42 kutoka vyama na mashirikisho ya michezo kutoka Tanzania Bara na Zanzibar walishiriki Mkutano huo Mkuu wa Kamisheni ya Wachezaji.

Baadhi ya vyama na mashirikisho hayo, ambayo kila moja lilileta wawakilishi wawili, wa kike na kiume ni pamoja na Judo, Riadha, Baseball, Softball, Chabata, Chabaza, Hockey, Trithlon, Mieleka, Mpira wa Mikono, Mpira wa Kikapu, Tenisi, Badminton na Shirikisho la Soka Zanzibar (ZFF).

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
gate 交易所
9 days ago

Great article! Your article helped me a lot. Thanks! What do you think? I want to share your article to my website: gate 交易所

Back to top button
1
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x